Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Peter Fitzek (59) amabaye alijitangaza kuwa mfalme wa Ujerumani na watawala wake watatu wamekamatwa na kundi lao kupigwa marufuku kwa kujaribu kupindua Serikali.
Peter Fitzek alikuwa miongoni mwa wale waliokamatwa katika uvamizi wa asubuhi kwenye majimbo saba Mwi 13, 2025 ambayo yalihusisha takribani maafisa 800 wa usalama.
Serikali ilipiga marufuku kikundi chao cha Reichsbürger,au ambao wanataka kuanzisha Königreich Deutschland, au Ufalme wa Ujerumani.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Alexander Dobrindt alilishutumu kundi hilo kwa kujaribu kudhoofisha utawala wa sheria kwa kuunda taifa mbadala na kueneza simulizi ya chuki dhidi ya Wayahudi ili kuunga mkono madai yao ya mamlaka.