Katika ibada maalum ya Sikukuu ya Pasaka, Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt. Fredrick Shoo, ametoa wito wa maridhiano ya kweli, uchaguzi huru na haki pamoja na kuheshimiwa uamuzi wa wananchi.
Akizungumza Aprili 20, 2025 katika Kanisa Kuu la Moshi Mjini, Askofu Shoo amesema,“tunaposema juu ya kuridhiana tunamaanisha, tunapotamka juu ya haki, amani na upeza leo ndo hatupaswi kuishia kwenye maneno tu ni lazima tuyatekeleze.”
Ameonya dhidi ya kurudia makosa ya chaguzi zilizopita, akitaka uchaguzi wa mwaka huu uwe wa wazi na unaoheshimu demokrasia huku akitoa rai kwa vyombo vya dola, kutojiingiza kwenye upendeleo wa kisiasa.
Aidha, amehimiza wananchi kuwa na hofu ya Mungu, kupenda nchi yao na kushiriki uchaguzi kwa ujasiri, wakiamini kuwa mabadiliko chanya yanawezekana.