DC Shaka Ahimiza Suala la Lishe Mashuleni Ataka Walimu,wazazi na Watendaji wa Kata Kujitoa

DC Shaka Ahimiza Suala la Lishe Mashuleni Ataka Walimu,wazazi na Watendaji wa Kata Kujitoa

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa  Shaka Hamdu Shaka, ametoa wito kwa wazazi, walimu, na watendaji wa kata kushirikiana kwa karibu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana shuleni.

Amesisitiza kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya elimu na afya kwa watoto, hivyo ni jukumu la kila mmoja katika jamii kuhakikisha suala hilo linapewa kipaumbele na kwamba hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila shule ina uwezo wa kuzalisha chakula chake, hivyo kuboresha lishe ya wanafunzi na kuongeza ufanisi katika elimu.

Shaka amebainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imejipanga kutumia rasilimali zilizopo, hususani ardhi yenye rutuba, kwa ajili ya kilimo cha chakula cha shule ambapo ametoa rai kwa watendaji wa kata ambao hawana maeneo ya kilimo kutoa taarifa ili wapatiwe ardhi kwa ajili ya shughuli hiyo muhimu.


Kikao hicho kimewashirikisha watendaji wa kata zote 40 pamoja na wataalam mbalimbali wa sekta ya lishe na elimu, DC Shaka amewataka watendaji hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuweka mkazo katika suala la lishe kwa wanafunzi huku akisisitiza kuwa agizo la kuhakikisha lishe bora kwa wanafunzi ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivyo ni lazima litekelezwe kwa vitendo.

Katika hatua nyingine DC  Shaka ameahidi kuwa wilaya ya Kilosa itaendelea kumuunga mkono  Rais kwa kuhakikisha kuwa suala la lishe kwa wanafunzi linapewa kipaumbele cha juu nakusema kuwa kwa kushirikiana na wazazi, walimu, na watendaji wa kata, watahakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata chakula cha mchana shuleni, hivyo kuboresha afya na ufaulu wao.

Related Articles

Visitor Counter

000530
Today: 4
Yesterday: 9
This Week: 40
Last Week: 32
This Month: 13

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz