Demokrasia Lazima Irejeshwe Kongo - Kabila

Demokrasia Lazima Irejeshwe Kongo - Kabila

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila amewataka raia wa nchi hiyo kupambana na kile amekiita "utawala wa udikteta" kwenye taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali.

Katika hotuba ya nadra alioitoa na kuirusha moja kwa moja kupitia mitandao, Kabila anayedhaniwa kuwa kwenye mojawapo ya nchi za kusini mwa Afrika amesema ni sharti "udikteta ukomeshwe, na demokrasia, hali nzuri ya uchumi na utawala unaowajali watu urejee" nchini Kongo.

Ingawa aliondoka nchini Kongo mwaka 2023, na hadi sasa hajulikani mahala alipo kiongozi huyo wa zamani ameendelea kuwa na ushawishi fulani kwenye rubaa za siasa za Kongo.

Kwenye hotuba yake hiyo ya Mei 23 2025, alioitoa siku moja baada ya Baraza la Seneti la Kongo kumwondolea kinga ya kushtakiwa, Kabila ameushambulia utawala wa Rais Felix Tshisekedi ikiwemo madai ya serikali mjini Kinshasa kuwa Rais huyo wa zamani aliingia nchini humo na yupo kwenye mji wa Goma unaoshikiliwa na waasi.

Uamuzi wa Seneti wa kumwondolea kinga Kabila unafungua njia ya uwezekano wa kiongozi huyo wa zamani kushtakiwa kwa kile serikali inasema kuwa ni uungaji wake mkono kwa kundi la waasi.

Mbali ya lawama kwa utawala wa Kongo, Kabila pia ameahidi atautembelea mji wa Goma hivi karibuni.

"Kufuatia tetesi za mtaani na mitandao ya kijamii, kuhusu uwepo wangu kwenye mji wa Goma, ambako nitakwenda siku chache zijazo utawala uliopo madarakani mjini Kinshasa uliamua kwa makusudi kulibeba suala hilo na dhamira ya kutia wasiwasi, hali inayodhihirisha demokrasia imeondoka nchini mwetu," amesema Kabila.

Related Articles

Visitor Counter

000969
Today: 14
Yesterday: 3
This Week: 17
Last Week: 49
This Month: 121

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz