EU  Mbioni kusitisha Uagizaji wa gesi  Kutoka  Urusi

EU Mbioni kusitisha Uagizaji wa gesi Kutoka Urusi

Tume ya Ulaya imechapisha ramani inayoelezea mipango yake ya kukomesha utegemezi wa Ulaya kwa nishati ya Urusi katika miaka ijayo.

Chini ya mipango hiyo, uagizaji wa gesi yote ya Urusi na gesi asilia ya kimiminika kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya utapigwa marufuku kufikia mwisho wa  mwaka 2027.

Kujibu mipango hiyo, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliliambia shirika la habari la Reuters siku ya Jumanne kwamba Ulaya ilikuwa ikijiwekea mazingira magumu yenyewe.

EU iliapa kusitisha uhusiano wake wa nishati na Urusi baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake nchini Ukraine mnamo 2022.

Vifungu vya mapendekezo ya kisheria vitawasilishwa mwezi Juni vikitaka nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya kufanya mipango ya kitaifa ya kukomesha uagizaji wa gesi ya Urusi na mafuta ya nyuklia kulingana na Tume ya Ulaya.

Nchi wanachama wa EU lazima ziwasilishe mikakati chini ya mipango ya kuchukua nafasi ya uagizaji wa mafuta ya Urusi ifikapo mwisho wa 2027.

Nchi pia zimetakiwa kueleza mikakati ya kukomesha utegemezi wao kwa Urusi kwa madini ya urani urani iliyorutubishwa na vifaa vingine vya nyuklia.

Related Articles

Visitor Counter

000970
Today: 1
Yesterday: 14
This Week: 18
Last Week: 49
This Month: 122

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz