Mwanasiasa wa mrengo mkali wa kulia anayependelea zaidi sera za kizalendo George Simion ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Romania uliofanyika siku ya Jumapili.
Kwenye uchaguzi huo, Simion wa chama cha Alliance for the Unity of Romanians (AUR), amejikingia asilimia 40.5 ya kura akiwazidi kwa umbali mkubwa wapinzani wake, ikiwemo Meya wa mji mkuu Bucharest Nicusor Dan aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 20.89 ya kura.
Kulikuwa na wagombea 11 kwenye uchaguzi huo na duru ya pili kutafuta mshindi atakayepata zaidi ya asilimia 50 itafanyika Mei 18.
Kufutwa kwa uchaguzi huo kuliitumbukiza Romania, taifa mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO kwenye mzozo mkubwa wa kisiasa kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa.