Kikosi Maalum cha Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran, kimetangaza vifo vya majenerali sita hali iliyoongeza idadi ya maafisa wakuu waliouawa katika kampeni ya kijeshi ya Israel kufikia watu wapatao16.
Miongoni mwa waliofariki Dunia ni mkuu wa kikosi hicho cha Walinzi wa Mapinduzi Hossein Salami na Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Iran Jenerali Mohammed Bagheri.
kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim lenye ushirikiano wa karibu na kikosi hicho cha Walinzi wa Mapinduzi, mazishi ya Salami, Bagheri na makamanda wengine, yanatarajiwa kufanyika Juni 17, 2025.
Majenerali hao wamefariki ndani ya siku tatu za mashambulizi ya anga ya Israel yanayolenga maeneo mbalimbali ya Iran, ikiwa ni pamoja na viwanda vya nyuklia, viongozi wa jeshi, mitambo ya ulinzi, miji na maeneo ya mafuta.
Iran imelaani mashambulizi hayo na imeyaita tangazo la vita, huku ikijibu kwa mashambulizi ya mamia ya makombora na droni ndani ya ardhi yaIsrael.