Israel imepinga uamuzi wa Umoja wa Ulaya kudurusu upya mkataba wake wa ushirikiano katika juhudi ya kuishinikiza kuhusiana na mashambulizi yake makali katika Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel Oren Marmorstein amesema katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa kijamii wa X kuwa wanakataa kabisa muelekeo uliochukuliwa katika taarifa hiyo, ambayo inaonyesha kutokuelewa kabisa ukweli kuhusu hali halisi ambayo Israeli inakabiliana nayo.
Mapema Mei 21 2025, Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas alisema katika taarifa kwamba umoja huo ulikuwa unatafakari kudurusu upya ushirikiano wake na Israel kwa kuzingatia operesheni mpya huko Gaza kufuatia mzingiro wa Israeli uliodumu wiki 11 katika eneo hilo.