Baraza la Seneti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limepiga kura ya kumuondolea kinga ya kutoshitakiwa rais wa zamani Joseph Kabila anayeshutumiwa na serikali kwa kuwasaidia waasi waliopo mashariki mwa Kongo.
Kura 88 zilipigwa kuunga mkono hatua hiyo itakayopelekea kiongozi huyo wa zamani kushitakiwa kwa kuwaunga mkono M23.
Spika wa Baraza la Seneti Jean-Michel Sama Lukonde alitangaza baada ya kura hiyo kwamba sasa baraza hilo limeruhusu Kabila kushitakiwa na kuondolewa kinga.
Rais Felix Tshisekedi aliyeshika usukani baada ya Kabila, anamtuhumu mtangulizi wake huyo kwa kushirikiana na M23 waliolikamata eneo kubwa la mashariki mwa Kongo.