Kesi ya mwanamke mmoja anayafahamika kwa jina la Erin Patterson (50) amabaye anashutumiwa kwa kuwauwa ndugu zake kwa uyoga wenye sumu wakati wa chakula cha mchana imeanza kusikilizwa ambapo mwanamke huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya mauaji shtaka moja likiwa ni kujaribu kuua kwa chakula cha mchana chenye sumu alichowapa ndugu zake huko Gippsland Kusini mnamo mwaka 2023.
Mahakama imesema kuwa Polisi hawajawahi kupata simu iliyotumika na Erin Patterson siku hiyo na simu nyingine iliyopatikana na kuchukuliwa wakati wanafanya msako nyumbani kwake ilikuwa imefutwa kila kitu na kurejeshwa ilivyokuwa mwanzoni.
Patterson pia aliwaambia polisi hajawahi kuwa na chombo cha kukausha chakula licha ya CCTV kumwonyesha akitupa kifaa hicho, na utafiti wa ujasusi baadaye ukaonyesha kuwa kifaa hicho kina alama za vidole vyake na kilipatikana na mabaki ya uyoga wenye sumu.