Kupunguzwa kwa bajeti za misaada kwawaweka hatarini wajawazito

Kupunguzwa kwa bajeti za misaada kwawaweka hatarini wajawazito

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa kupunguzwa kwa bajeti za misaada kutahujumu hatua zilizokuwa zimefanikishwa za kupunguza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua.

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema vifo vitokanavyo na ujauzito na kujifungua vilikuwa vimeshuka kwa asilimia arobaini katika karne hii lakini wataalam wanahofu kuwa huwenda vifo hivyo vikaongezeka tena kutokana na kusitishwa kwa misaada ya kigeni.

Wanawake walio na ujauzito hukumbwa na changamoto nyingi hasa katika mataifa yanayokumbwa na mizozo kama Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nigeria na Somalia.

Mnamo mwaka 2020,WHO ilirekodi vifo zaidi ya  laki mbili  ikiwa ni sawa na mwanamke mmoja kufariki Dunia kila baada ya dakika mbili kutokana na changamoto wakati wa kujifungua.

Kifo cha uzazi ni kile kinachosababishwa na matatizo wakati wa ujauzito au ndani ya wiki sita baada ya mwisho wake huku sababu zinazoongoza katika vifo hivyo ikiwa  ni pamoja na kutokwa na damu nyingi, maambukizi kama vile malaria, matatizo wakati wa kujifungua, na utoaji mimba usio salama.

Related Articles

Visitor Counter

000549
Today: 5
Yesterday: 5
This Week: 5
Last Week: 54
This Month: 32

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz