Maandamano Yazidi Kushika Kasi  Los Angeles

Maandamano Yazidi Kushika Kasi Los Angeles

Katika hali ya kusitaajabisha maandamano yamezidi kupamba moto kwa siku ya tatu huko Los Angeles  nchini Marekani ambako waandamanaji wanaopinga sera za uhamiaji za Rais wa Marekani Donald Trump wamekabiliana na maafisa wa usalama.

Wanajeshi wa kikosi maalum waliotumwa na Rais Trump mjini humo licha ya pingamizi kutoka kwa Gavana wa jimbo la California na Meya wa mji wa Los Angeles, wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kukabiliana na waandamanaji hao.

Meya wa Los Angeles Karen Bass amesema machafuko katika jiji hilo yaliyochochewa na utawala huku Gavana wa California Gavin Newsom akisema kuwa uamuzi wa Donald Trump kupeleka Walinzi wa Kitaifa kwenye maandamano hayo ndio uliozidisha ghasia hizo.

Waandamanaji walikusanyika karibu na eneo ambapo maafisa wa uhamiaji na utekelezaji wa Forodha walifanya uvamizi siku ya Juni 7, 2025  na kufunga barabara kuu .

 

 

Related Articles

Visitor Counter

000969
Today: 14
Yesterday: 3
This Week: 17
Last Week: 49
This Month: 121

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz