Rais William Ruto wa Kenya ameomba radhi kwa nchi majirani ambazo ni Tanzania na Uganda kufuatia kile alichosema malumbano yanayoendelea katika mitandao ya kijamii yanayofanywa na vijana wachache wa nchi hiyo yaliyodumu kwa muda wa wiki mbili sasa baada ya wanaharakati kadhaa wa nchi hiyo kuzuiliwa kuingia Tanzania.
Rais Ruto ametoa kauli hiyo leo Mei 28, 2025, alipokuwa akilihutubia Taifa wakati wa maombi ya Kitaifa.
"Tunataka kutembea hii safari pamoja, kujenga mahusiano kwa misingi ya kuheshimiana na kuelewana,"
"Kwa majirani zetu Tanzania, ikiwa tumewakosea kwa vyovyote vile, tunaomba radhi kwa mioyo yetu yote. Tafadhali tusameheni. Kwa ndugu na dada zetu Uganda, ikiwa kuna vile tumewaendea visivyo, tunaomba msamaha wenu." Amesema Rais Ruto

See translation