Rais wa Marekani,Donald Trump ameamuru bendera zote zipandishwe nusu mlingoti kama sehemu ya maombolezo ya Baba Mtakatifu Francis, aliyefariki jana Jumatatu Aprili 21, 2025
Amri hii inahusisha “majengo yote ya umma na maeneo, katika kila kituo cha kijeshi na vituo vya baharini na kwenye meli zote za baharini za Serikali ya Shirikisho katika Wilaya ya Columbia na katika sehemu zote za Marekani na miliki zake hadi jua litakapotua, siku ya maziko,” taarifa ilieleza.
Taarifa iliongezea kuwa, “ amri hiyo inajumuisha balozi za Marekani, ofisi za kidiplomasia, ofisi za konsula, na vituo vingine vya nje, ikiwa ni pamoja na vifaa vyote vya kijeshi na meli za baharini na vituo pia vinahusika”.
