Mataifa ya Ulaya Mbioni  Kuongeza Vikwazo Dhidi ya Urusi

Mataifa ya Ulaya Mbioni Kuongeza Vikwazo Dhidi ya Urusi

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Poland na Uhispania na mwakilishi wa EU wamejadili jinsi ya kuendelea kuiunga mkono Ukraine dhidi ya Urusi katika mkutano uliofanyika mjini London.

Wanadiplomasia hao wameituhumu Ikulu ya Kremlin kwa kile walichokiita kufanya michezo kuhusu mazungumzo ya amani na Ukraine.

Katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano wao katika mji mkuu wa Uingereza, mawaziri hao wa mambo ya nje wameeleza wasiwasi wao kwamba Urusi haijaonyesha nia ya dhati ya kupiga hatua.

Mawaziri hao kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Poland, Uhispania na Umoja wa Ulaya wamesema katika tamko la pamoja kwamba Urusi lazima ikubali mpango wa kusitisha mapigano bila kuchelewa.

Moscow kwa upande wake imepuuzilia mbali shinikizo kutoka kwa viongozi wa Ulaya la kuitaka kuukubali mpango wa kusitisha mapigano kwa siku 30 bila masharti yoyote kuanzia jana Jumatatu, ikisema Urusi haitakubali vitisho.

 

Related Articles

Visitor Counter

000970
Today: 1
Yesterday: 14
This Week: 18
Last Week: 49
This Month: 122

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz