Mkutano wa G7 Waijadili Ukraine na Uchumi wa Dunia

Mkutano wa G7 Waijadili Ukraine na Uchumi wa Dunia

Mkutano wa nchi zilizositawi kiviwanda Duniani G7 unajadili hali ya uchumi wa dunia na mzozo wa vita vya Ukraine mkutano huo unawalea pamoja mawaziri wa fedha wa nchi za G7 na magavana wa benki kuu.

Mawaziri wa fedha wa nchi zilizostawi kiviwanda Duniani G7 wanaendelea na mkutano wao leo ulionaza jana nchini Kanada katika mazungumzo yanayotarajiwa kugubikwa na wasiwasi wa kiuchumi unaotokana na ushuru uliowekwa na Rais wa Marekani Donald Trump huku wasiwasi kuhusu vita vya Ukraine ukiendelea kupewa kipaumbele.

Waziri wa fedha wa Kanada Francois-Philippe Champagne amesema watajaribu kukubaliana kuhusu sera za kurejesha ukuaji na uthabiti wa uchumi huku akikiri kuwa wasiwasi kuhusu ushuru mpya wa Marekani utaendelea.

Katika mikutano itakayoendelea hadi kesho Alhamisi viongozi watajadili hali ya uchumi duniani, huku washiriki wakitafuta msimamo wa pamoja kuhusu Ukraine.

Masuala kama uhalifu wa kifedha na desturi zisizo za masoko pia yako kwenye ajenda.

Waziri wa fedha wa Ukraine Sergii Marchenko anahudhuria mkutano huo wa mawaziri wa fedha wa nchi za G7 na magava wa benki kuu unaofanya katika jimbo la Alberta, magharibi mwa Kanada.

Related Articles

Visitor Counter

000972
Today: 3
Yesterday: 14
This Week: 20
Last Week: 49
This Month: 124

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz