Mahakama kuu huko Abuja nchini Nigeria imemhukumu Peter Nwachukwu, mume wa mwimbaji maarufu wa injili Osinachi, adhabu ya kunyongwa hadi kifo baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.
Hukumu hiyo, iliyotolewa na jaji Nwosu-Iheme, imetolewa miaka mitatu baada ya kifo cha osinachi kilichotokea mnamo aprili 8, 2022. Kesi hiyo imejulikana zaidi kwa sababu ya umaarufu wa Osinachi katika muziki wa injili wa Nigeria na jamii ya wakristo.
Polisi walikuwa wamemkamata bwana nwachukwu baada ya mkewe, kufariki akiwa katika hospitali moja huko Abuja huku ripoti za awali zikiwa zimependekeza kuwa mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 42 alikuwa mgonjwa wa saratani ya koo, lakini familia yake ilikataa na kudai kwamba alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.