Mwaka 2025 Umewaendea Vizuri Wakulima wa Pamba

Mwaka 2025 Umewaendea Vizuri Wakulima wa Pamba

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema mwaka huu wa 2025 Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha mbolea, viuatilifu na mbegu za pamba zitolewe bure kwa wakulima wa zao la pamba.

Waziri Bashe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Samia na wananchi wa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, uliofanyika kwenye Viwanja vya Stendi ya Meatu leo Juni 17, 2025.

“Mwaka huu Mheshimiwa Rais umenipa idhini ya kuwaletea wakulima wa pamba mbolea maalumu ambayo tutaanza kuigawa mwezi wa 10 kwa ajili ya kutumika kwenye zao la pamba, na mbolea hii itagawiwa bure kwa wakulima wa pamba,” amesema Waziri Bashe

Ameongeza kuwa pamoja na kupata mbegu hizo bure, wakulima hao pia watapata viuatilifu bure na mbegu bure.

“Kwa hiyo mkulima wa pamba mwaka huu atapata mbegu bure, atapata kiuatilifu bure, atapata huduma ya trekta kwa bei ya ruzuku na mbolea bure kwa zao la pamba,” amesema Waziri Bashe

Related Articles

Visitor Counter

000968
Today: 13
Yesterday: 3
This Week: 16
Last Week: 49
This Month: 120

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz