Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Constant Mutamba, anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya takriban dola milioni 20 za Marekani, ambazo zilikuwa zimekusudiwa kwa ajili ya kufidia waathirika wa vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa hizo zilitolewa jana na Spika wa Bunge la DRC, Vital Kamerhe, ambaye amesema kuwa bunge limeanzisha mchakato wa kumhoji Waziri Mutamba kupitia tume maalum ya uchunguzi, ambayo itaundwa na wabunge watakaotangazwa hivi karibuni.
“Tumeunda tume maalum ya kibunge kwa ajili ya kumhoji Waziri wa Sheria kuhusu tuhuma hizi nzito zinazohusu fedha zilizotengwa kwa fidia ya waathirika wa migogoro ya kijeshi mashariki,” alisema Kamerhe.
, Constant Mutamba, anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya takriban dola milioni 20 za Marekani, ambazo zilikuwa zimekusudiwa kwa ajili ya ku.jpg)