Rais Donald Trump ametangaza kumteua mshauri wake wa usalama wa kitaifa, Mike Waltz, kuwa balozi wa Marekani katika Shirika la Umoja wa Mataifa.
Trump ametoa tangazo hilo Mei mosi 2025, kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social huku Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio akatarajiwa kushika nafasi ya Mike Waltz kwa muda.
Tangazo hilo lilitolewa saa chache kufuatia ripoti kuwa Waltz na naibu wake, Alex Wong, watajiuzulu nafasi zao, wakati shinikizo likizidi kuhusu jukumu la Waltz kwenye kashfa ya Signalgate.
Waltz alimuunga bila kukusudia mwandishi wa habari kwenye kundi ambalo hujadiliana taarifa za siri hususani za mipango ya vita, hatua iliyobua madai ya taarifa hizo kuvuja