Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa wakazi wa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, kufuatia vifo vya vijana wanne waliofariki dunia katika ajali ya barabarani walipokuwa njiani wakielekea kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi ya Mabasi ya Meatu leo Juni 17, 2025 ambapo yeye alikuwa akihutubia.
Mbali na vijana hao wanne kufariki dunia, watu wengine waliojeruhiwa katika ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu.
“Kabla sijaendelea ndugu zangu nitoe pole nyingi sana, tumepoteza vijana wetu wanne lakini na wengine kadhaa wameumia katika usafiri kuja kwenye mkutano huu. Nitoe pole sana kwa wana Meatu,” amesema Rais Samia
Mbali na kutoa salamu za pole, Rais Samia Suluhu Hassan amefika katika Hospitali ya Wilaya Meatu ili kuwajua hali majeruhi wa ajali hiyo wanaoendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
