Rais Trump Azuia Raia kutoka Nchi 12 Kuingia Marekani

Rais Trump Azuia Raia kutoka Nchi 12 Kuingia Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini tangazo la kupiga marufuku raia wa mataifa 12 kuingia nchini humo ambapo Katika awamu yake ya kwanza Trump aliwazuia watu kutoka mataifa saba yenye Waislamu wengi kuingia Marekani.

Tangazo hilo  linawazuia kabisa na kuwawekea mipaka raia wa mataifa hayo kuingia nchini Marekani  huku Mataifa hayo yakiwa ni Afghanistan, Myanmar, Chad, Kongo, Guinea ya Ikweta, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen, hii ikiwa ni kulingana na kituo cha utangazaji cha CBS.

Aidha raia wa mataifa mengine saba ya Burundi, Cuba, Laos, Sierra Leone, Togo, Turkmenistan na Venezuela watawekewa zuio la kiwango fulani.

Wakati wa muhula wake wa kwanza, Trump aliwapiga marufuku wasafiri kutoka mataifa saba yenye idadi kubwa ya Waislamu kuingia Marekani, hatua ambayo hata hivyo ilipata ukinzani wa kisheria.

Katika hatua nyingine, Trump ameagiza uchunguzi kuhusu kile ambacho wanasiasa wa chama chake cha Republican wanadai kuwa ni kufichwa kwa hali ya afya ya mtangulizi wake Joe Biden alipokuwa madarakani.

Related Articles

Visitor Counter

000969
Today: 14
Yesterday: 3
This Week: 17
Last Week: 49
This Month: 121

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz