Cyril Ramaphosa Kukutana na Rais wa Marekani Wiki Ijayo

Cyril Ramaphosa Kukutana na Rais wa Marekani Wiki Ijayo

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa  anatarajia kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump wiki ijayo nchini Marekani katika  ziara rasmi.

Trump amekata misaada yote ya kifedha ya Marekani kwa Afrika Kusini, akikosoa sera yake ya mageuzi ya umiliki wa ardhi na kesi ya mauaji ya halaiki ambayo Afrika Kusini iliiwasilisha katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC dhidi ya Israel, nchi ambayo ni mwandani wa Marekani.

Wiki hii utawala wa Trump uliwakaribisha Marekani, Waafrika Kusini 49 weupe, ukisema wamekuwa wahanga wa ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini huku Serikali ya Afrika Kusini ikikanusha madai ya Trump ikisema hakuna ushahidi wa kuteswa kwa Waafrika Kusini weupe nchini humo.

Related Articles

Visitor Counter

000970
Today: 1
Yesterday: 14
This Week: 18
Last Week: 49
This Month: 122

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz