Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi MaryPrisca Mahundi amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imeendelea kuimarisha mifumo ya mawasiliano ili kudhibiti vitendo vya utapeli mitandaoni.
Akijibu maswali bungeni jijini Dodoma, Mhandisi Mahundi amesema huduma mbalimbali zimeanzishwa na zimekuwa na mafanikio katika kuwanasa watu wanaodaiwa kuhusika na utapeli wa mtandaoni unaowaathiri Watanzania.
“Watanzania wachukue tahadhari, waache kuwasiliana na watu wasiowafahamu wapuuzeni ,” alisisitiza Injinia Mahundi.
