Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), kwa kushirikiana na wadau kutoka nje ya nchi, inatarajia kujenga kiwanda cha kisasa cha uchapishaji wa vitabu, ikiwa ni juhudi za kupunguza gharama za uchapishaji nchini.
Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya TET yatakayofanyika Juni 17, mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba amesema.
“Tumeazimia kujenga kiwanda kikubwa cha uchapishaji eneo la Mikocheni kwa kushirikiana na wadau kutoka nje ya nchi ili kupunguza gharama za uchapishaji,” amesema Dk. Komba.
Dk. Komba aliongeza kuwa uwekezaji huo utaiwezesha TET kuzalisha vitabu kwa wingi na kwa wakati, hali itakayochangia katika kuboresha upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia nchini.
