Trump Aridhishwa na Kusifu mazungumzo  Kati ya Marekani na China

Trump Aridhishwa na Kusifu mazungumzo Kati ya Marekani na China

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kumekuwa na marekebisho katika uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na China kufuatia siku ya kwanza ya mazungumzo kati ya maafisa wa Marekani na China nchini Uswizi.

Katika chapisho la mtandao wa kijamii Rais  huyo wa Marekani alielezea mazungumzo hayo kuwa mazuri sanana kusema mabadiliko yamejadiliwa kwa njia ya kirafiki,  na yenye kujenga

Vita vya kibiashara vinavyoongezeka kati ya Washington na Beijing vimeshuhudia Rais wa Marekani akipinga bidhaa za China zinazoingia Marekani kwa ushuru wa 145%.

China ililipiza kisasi kwa ushuru wa 125% kwa baadhi ya bidhaa za Marekani.

Kufuatia miezi kadhaa ya piga nikupige, nchi hizo mbili zimekutana huko Geneva wikendi hii kwa mara ya kwanza tangu Trump aipige China kwa ushuru mwanzoni mwa mwaka.

Taarifa chache zaidi kwenye chapisho la jukwaa la kijamii la Truth ni kuwa mazungumzo yanatarajiwa kuendelea leo Mei 11, 2025 na yanafanyika kati ya makamu mkuu wa China He Lifeng na Waziri wa Hazina wa Marekani Scott Bessent.

 

Related Articles

Visitor Counter

000972
Today: 3
Yesterday: 14
This Week: 20
Last Week: 49
This Month: 124

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz