Ufugaji wa Samaki Kwenye Vizimba Unaua Wavuvi Njaa

Ufugaji wa Samaki Kwenye Vizimba Unaua Wavuvi Njaa

Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba amedai kuwa uwekezaji unaofanywa na raia wa kigeni kwa kufuga samaki kwenye vizimba Ziwa Victoria unaleta athari kubwa kwa jamii inayotegemea samaki kujiendesha kiuchumi.

Ametoa kauli hiyo leo Juni 13, 2025 kwenye mdahalo wa uchambuzi wa bajeti ya mwaka 2025/26 uliofanyika Ukumbi wa Msekwa, bungeni mjini Dodoma,ukihusisha wabunge na wataalamu wa mambo ya uchumi na fedha kutoka Wizara ya Fedha, Benki Kuu (BoT) na Tume ya Taifa ya Mipango, ambao waliwasilisha mada na kisha wabunge kuchangia.

Kishimba amedai kuna raia wa China anaendesha vizimba na anapata samaki wengi kwa siku ambao anawaingiza kwenye soko la kawaida, ambalo wavuvi wengine pia hulitegemea.

Amedai kuwa raia huyo peke yake anatengeneza karibu Sh Mil. 300 kwa siku, jambo ambalo linafanya wavuvi wengine kukosa soko, hivyo kuomba mamlaka husika zifanye utafiti kuhusu ufugaji samaki kwenye Ziwa Victoria na kuangalia kama nchi nyingine zinafanya hivyo au unafanyika kwenye mito pekee.

Pia alilamikia kuhusu vyakula ambavyo samaki hao wanakula, akisema vinawafanya samaki wanaofugwa wasizae, lakini chakula hicho kinadondoka pia ziwani hivyo samaki wengine nao wanakula na kuhoji kama hakutakuwa na athari kwa samaki wasiofugwa.

Related Articles

Visitor Counter

000968
Today: 13
Yesterday: 3
This Week: 16
Last Week: 49
This Month: 120

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz