Waziri wa zamani wa Sheria nchini Kenya Martha Karua amesema anadhani uhuru wa raia katika eneo la Afrika Mashariki unadorora.
Karua amewatuhumu viongozi wa mataifa matatu ya ukanda huo ambayo ni Tanzania, Kenya na Uganda kushirikiana kuwakandamiza raia.
Amesema hayo alipozungumza na moja ya chombo cha habari.
Amesema kuwa watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wana jukumu la kushikamana ili kuhakikisha wanadhoofisha mielekeo ya kimila na ukiukwaji wa haki.
Karua alizuiwa kuingia Tanzania mapema wiki hii, alipokuwa akienda kuhudhuria kesi dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha CHADEMA, Tundu Lissu, kama mwangalizi.
Kwa sasa Karua anamwakilisha mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye pia anatuhumiwa kwa uhaini.