Waziri wa zamani wa Sheria nchini Kenya Martha Karua amesema anadhani uhuru wa raia katika eneo la Afrika Mashariki unadorora.
Karua amewatuhumu viongozi wa mataifa matatu ya ukanda huo ya Tanzania, Kenya na Uganda kushirikiana kuwakandamiza raia.
Amesema hayo alipozungumza na moja ya chombo cha habari.
Amesema kuwa anadhani watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wana jukumu la kushikamana ili kuhakikisha wanadhoofisha mielekeo ya kimila na ukiukwaji wa haki.
Karua alizuiwa kuingia Tanzania mapema wiki hii, alipokuwa akienda kuhudhuria kesi dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha CHADEMA, Tundu Lissu, kama mwangalizi.
Lissu anakabiliwa na mashitaka ya uhaini na uchochezi.
Kwa sasa Karua anamwakilisha mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye pia anatuhumiwa kwa uhaini.