viongozi wa ngazi za juu wa Marekani, umoja wa Ulaya na Ukraine, wanatarajia kukutana alhamisi mjini Paris nchini Ufaransa , kujadili hatma ya mzozo kati ya Urusi na Ukraine na kukwama kwa juhudi za amani.
mkutano huo utahudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, mjumbe maalum wa Rais wa Marekani , Steve Witkoff, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri wake wa mambo ya nje Jean-Noel Barrot.
Ukraine itawakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje Andrii Sybiha pamoja na mkuu wa ofisi ya rais Andriy Yermak ambaye amesema watakutana pia kwa mazungumzo na viongozi wa Ujerumani na Uingereza kuhusu suala la dhamana ya usalama ikiwa kutafikiwa mpango wa amani.