Waafrika Watatu Wanaotajwa Katika Uchaguzi wa Papa

Waafrika Watatu Wanaotajwa Katika Uchaguzi wa Papa

Kongamano ambalo limepigiwa kura na Makadinali wa Kanisa Katoliki kumchagua Papa mpya, limeanza vikao mnamo Mei 7 2025 huku vikao vya faragha vikifanyika katika Kanisa la Sistine na kuhudhuriwa na  Makadinali  wapatao 135.

Haijulikani itachukua muda gani kumchagua Papa, lakini mikutano miwili ya awali iliyofanyika mwaka 2005 na 2013, ilidumu kwa siku mbili pekee.

 

Wakiwa ndani ya kanisa la Sistine, Makadinali hawatakiwi kuwasiliana na ulimwengu wa nje hadi Papa mpya atakapochaguliwa.

Kuna duru moja tu ya upigaji kura siku ya kwanza katika majira ya alasiri. Kuanzia siku ya pili na kuendelea, Makadinali hupiga kura mara mbili kila asubuhi na mara mbili kila alasiri katika kanisa.

Ili kuchaguliwa kuwa Papa, mgombea lazima apate thuluthi mbili ya kura za wapiga kura Makardinali.

Wakati wa kupiga kura, kila mpiga kura huandika jina la mgombea anayempendelea kwenye karatasi ya kura chini ya maneno "Ninamchagua kama Papa Mkuu."

Ili kuhifadhi usiri wa kura, Makadinali huagizwa kutotumia mwandiko wao wa kawaida. Iwapo hakuna kura ya uamuzi kufikia mwisho wa siku ya pili, siku ya tatu inatolewa kwa sala na kutafakari, bila kura yoyote kufanyika. Upigaji kura unaendelea kama kawaida baada ya siku hiyo. Mchakato wote unaweza kuchukua siku kadhaa au hata wiki.

Mara mbili kwa siku, kura huchomwa, na watu walio nje ya Vatikani huona moshi ukitoka kwenye bomba la Kanisa la Sistine.

Wino mweusi au mweupe huwekwa kwenye kura. Moshi mweusi unamaanisha kura bado haijaamua. Moshi mweupe unaonyesha Papa amepatikana.

Makardinali watapigia kura wagombea hadi jina moja litokee. Huku asilimia 80 ya Makadinali wakiteuliwa na Papa Francis, hii ni mara yao ya kwanza kumchagua Papa na watafanya hivyo kwa mtazamo mpana wa kimataifa.

Kwa mara ya kwanza katika historia, chini ya nusu ya Makadinali wapiga kura ndio wanatokea Ulaya. Brazil ina wawakilishi saba katika kundi hili.

 

Related Articles

Visitor Counter

000970
Today: 1
Yesterday: 14
This Week: 18
Last Week: 49
This Month: 122

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz