Mamilioni ya raia wa Korea Kusini wamepiga kura ya kumchagua rais mpya wa nchi hiyo atakayerithi mikoba ya Yoon Suk Yeol
Rais mpya wa nchi anatazamiwa kurithi mikoba ya Yoon Suk Yeol aliyeondolewa kutokana na agizo lake la kuiweka nchi chini ya sheria ya kijeshi mwishoni mwa mwaka uliopita.
Hadi sasa duru zinasema kiongozi wa upinzani wa mrengo wa kushoto Lee Jae-myung ndiye aliyeko katika nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi huo.
Mgombea mkuu wa kihafidhina, Kim Moon Soo, anashikilia nafasi ya pili na mshindi anaweza kutangazwa Juni 4, 2025
Uchaguzi huu utaamua hatima ya demokrasia ya Korea Kusini ingawa wachambuzi wana wasiwasi kuwa mgawanyiko wa ndani uliosababishwa na rais Yoon Suk Yeol bado haujaisha na unaweza kuendelea kuitibua nchi hiyo hata baada ya kupatikana kwa Rais mpya.