Viongozi wastaafu barani Afrika pamoja na wataalam wa maendeleo wametoa wito kwa Serikali barani humo kutekeleza mikakati inayotambua na kutoa motisha kwa watu wanaowekeza katika juhudi za uhifadhi wa mazingira.
Wito huo umetolewa Aprili 8,2025 katika Jiji la Kampala nchini Uganda katika siku ya pili ya Mkutano wa 8 wa Viongozi wa Afrika (ALF), unaoendelea chini ya uratibu wa Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute).
Mlezi wa Kongamano hilo na Rais wa Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amesisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika kuwawezesha wananchi wao, hususani wataalam wa majadiliano wa masuala ya mazingira ili waweze kushiriki kikamilifu katika majukwaa ya kimataifa.
“Tunaponyimwa fursa ya kutumia ipasavyo rasilimali zetu na badala yake zikanufaisha mataifa yenye nguvu kiuchumi, tunajikuta tukikosa uwezo wa kushughulikia changamoto kama mabadiliko ya tabia nchi na uhifadhi wa misitu”
“Tunatoa motisha kwa watu wanaopanda miti mipya lakini hatuwatambui wala kuwathamini wale wanaolinda misitu iliyopo. Hii inaleta pengo kubwa katika juhudi za uhifadhi na kudhoofisha azma ya kulinda ikolojia ya asili.” amesema Rais mstaafu Kikwete.
Amesisitiza kuwa mfumo wa sasa ambao unamnufaisha kifedha mharibifu wa mazingira huku mhifadhi akikosa chochote hauwezi kudumu. “Ni lazima mataifa hayo yabadilishe mtazamo huu kwa kutambua mchango wa misitu katika kuhifadhi kaboni.
