Waziri wa Zamani wa Fedha wa Ghana Awekwa Kwenye Orodha ya Uhalifu

Waziri wa Zamani wa Fedha wa Ghana Awekwa Kwenye Orodha ya Uhalifu

Waziri wa zamani wa fedha wa Ghana Ken Ofori-Atta amewekwa kwenye orodha ya uhalifu ya Interpol kwa madai ya kutumia ofisi ya umma kujinufaisha binafsi.

Haya yamejiri baada ya waendesha mashtaka wa Ghana kutangaza kuwa  waziri huyo anasakwa kwa  sheria, kwa madai ya kuhusika katika kesi kadhaa za ufisadi alipokuwa serikalini.

Notisi hii sio hati ya kukamatwa bali ni ombi kwa polisi ulimwenguni kote kumzuia mtu anayesubiri kurejeshwa. Ofori-Atta anayedaiwa kuwa nje ya nchi kwa sababu za kimatibabu, hajazungumzia tuhuma hizo, lakini amesema ametendewa kinyume cha sheria.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 65 ameshutumiwa kwa kusababisha hasara ya kifedha kwa serikali.

Madai hayo yanajumuisha maswali kuhusu taratibu za ununuzi katika jengo la kanisa kuu la kitaifa lenye utata, ambalo limesalia kuwa shimo licha ya madai ya matumizi ya $58m (£46.6m) ya pesa za Serikali.

Mawakili wa Ofori-Atta walikuwa wamejitolea kumwakilisha lakini mwendesha mashtaka wa serikali alisema hawakuweza kujibu mashtaka ya jinai kwa niaba ya mteja wao.

Related Articles

Visitor Counter

000969
Today: 14
Yesterday: 3
This Week: 17
Last Week: 49
This Month: 121

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz