Marekani imetangaza kupunguza msaada wa $50m (£37m) kwa sekta ya afya ya Zambia, kutokana na nchi hiyo kushindwa kushughulikia wizi wa kimfumo wa dawa na vifaa tiba vilivyotolewa.
Uamuzi huu mgumu ulichukuliwa baada ya onyo la mara kwa mara kwa Serikali ya Zambia kulinda dawa muhimu kwa ajili ya wagonjwa walio hatarini zaidi nchini humo,
Hatua hii ya Marekani kwa Zambia ni tofauti na kusitishwa kwa misaada ya kigeni iliyotangazwa na Rais Donald Trump mnamo Januari.
Zaidi ya maduka ya dawa 2,000 kote nchini Zambia yalipatikana yakiuza dawa na vifaa tiba vilivyotolewa katika uchunguzi wa mwaka mzima uliofanywa na ubalozi wa Marekani.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya taarifa vimeeleza kuwa kwa hali ya kushangaza, asilimia 95 ya maduka ya dawa yaliyokuwa yakiuza aina ya bidhaa ambazo Marekani hutoa, pia walikuwa wakiuza bidhaa za wizi.
Takribani nusu ya maduka ya dawa yaliyotembelewa yalipatikana yakiuza dawa na vifaa vilivyotolewa na serikali ya Marekani hukun maduka mengine ya dawa pia yalikuwa yakiuza hisa za matibabu zilizoibiwa na kununuliwa na serikali ya Zambia, Mfuko wa dunia na wafadhili wengine.