Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kimedai Jeshi la Polisi kuendesha operesheni haramu ya kuzingira na kuvamia makazi ya viongozi wa chama hicho ambao ni Mwenyekiti wa Chama Mh. Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho. Mh. John Heche
Kwa mujibu wa Taarifa iliyo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi Bi. Brandina Rupia imeeleza kuwa Katika makazi ya Mhe. Tundu Lissu, Askari wa Jeshi la Polisi wamevamia makazi ya Mh Lisu wakitaka kufanya upekuzi wa nyumba (upekuzi usiofuata sheria na taratibu), huku wakitumia lugha za vitisho na vitendo vinavyokiuka misingi ya kisheria na haki za binadamu.
Aidha taarifa hiyo imepinga kwa nguvu zote uvunjaji huo wa sheria na taratibu na kutaka majibu ya haraka kwa maswali sita waliouliza Jeshi la Polisi na Serikali ya CCM:
1. Kwa nini walitaka kufanya upekuzi usiku wa manane kama majambazi badala ya mchana kwa uwazi na kufuata taratibu na sheria?
2. Kwa nini hawakuonesha hati halali ya upekuzi kutoka mahakamani (Search Warrant) kama sheria inavyotaka?
3.Kwa nini hawakuambatana na kiongozi wa mtaa ili kushuhudia upekuzi kama taratibu na sheria zinavyowataka?
4. Kwa nini mnapanga kutekeleza au kufanya upekuzi katika nyumba ambayo mmiliki wake yupo gerezani na hawezi kushuhudia?
5. Je, Jeshi la Polisi linakusudia kumuweka Mhe. John Heche chini ya kifungo




Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa vigezo sita vya kuzingatiwa na taasisi za kiraia zinazotarajia kutoa elimu ya mpiga kura na uraia kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
INEC pia ilizitaka taasisi zinazotaka kutoa elimu ya mpiga kura na uraia kutuma maombi yao kuanzia jana Aprili 21, 2025 hadi Mei 20, 2025 ambapo taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima ya Aprili 19, 2025 iliyotolewa jana ilieleza kuwa mwaliko huo umetolewa kwa kuzingatia kufungu cha 10 (1) (g) na (h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Namba 2 ya 2024.
“Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha Aprili 3, 2025 imetoa mwaliko kwa taasisi na asasi za kiraia zenye nia ya kutoa elimu ya mpiga kura na uangalizi wakati wa uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani 2025,” alisema.
INEC ilibainisha vigezo hivyo ni taasisi na asasi kusajiliwa na sheria za Tanzania, taasisi na asasi hizo kufanya kazi kwa kipindi kisichopungua miezi sita tangu kusajiliwa kwake.
Pia, kwa taasisi zenye watendaji wa kimataifa, INEC ilisema ni lazima watendaji wawili wakuu kati ya watatu wawe raia wa Tanzania.
Tume ilieleza kuwa taasisi au asasi hizo hazipaswi kujihusisha na uchochezi au kuvuruga amani katika utendaji wake na zinatakiwa kuwa na uzoefu wa kutoa elimu ya mpigakura na iwe tayari kujigharamia katika kutoa Elimu ya Mpigakura.
Aidha, tume pia ilisema taasisi na asasi zitakazo tuma maombi ya uangalizi wa uchaguzi wanapaswa kuzingatia masharti yaliyopo kwenye mwongozo wa uchaguzi mkuu.
Asasi za kiraia na taasisi hizo zinapaswa kuainisha anuani ya taasisi au asasi zao, mahali taasisi au asasi husika inapofanyia kazi, shughuli zinazofanywa na taasisi au asasi husika kwa mujibu wa hati ya usajili.
Aidha, zinapaswa kuainisha mahali taasisi hizo inatarajia kwenda kuangalia uchaguzi huo, idadi, majina, na taarifa binafsi za watendaji wa taasisi au asasi zitawatumia katika usimamizi na uangalizi.
Pia, taasisi na asasi za kiraia zinatakiwa kuwasilisha majina na namba za simu za viongozi wao.
Pia, asasi hizo zinatakiwa kuambatanisha nakala vivuli na nyaraka ya usajili wa taasisi au asasi husika na nakala kivuli ya Katiba ya taasisi au asasi husika.
Tume ilieleza maombi hayo yanapaswa kutumwa katika mfumo wa Kusajili Watazamaji, Asasi za Kiraia na Vyombo vya Habari na ilisisitiza kuwa maombi yatakayotumwa kwa njia tofauti na mfumo ulioainishwa hayatafanyiwa kazi.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amefanya ziara ya kukagua hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu la kukipandisha hadhi Kituo cha Afya cha Mama Ngoma kuwa hospitali ya ngazi ya juu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Mollel amesema kuwa ameridhishwa na maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa, na amesisitiza umuhimu wa mshikamano kati ya serikali na sekta binafsi katika kuboresha huduma kwa wananchi. “Tupo hapa kuhakikisha kilichoelekezwa na Waziri Mkuu kinatekelezwa kwa vitendo. Serikali haishindani na sekta binafsi bali tunashirikiana kutoa huduma bora kwa jamii,” amesema Dkt. Mollel.
Kwa upande wake, Profesa Ngoma ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wa kituo hicho katika jamii na kukipa kipaumbele. “Hili si jambo kwa ajili ya mtu mmoja, ni kwa manufaa ya wananchi wote wa eneo hili na maeneo ya jirani,” amesema Profesa huyo..
Uwepo wa Hospitali ya Mama Ngoma katika eneo la Kwangoa umetajwa kuwa muhimu kutokana na umbali wa hospitali ya wilaya, hivyo kusaidia kupunguza gharama za Serikali na kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.
- Askofu Dkt. Shoo Aonya dhidi ya Kurudia Makosa ya Chaguzi zilizopita atoa rai kwa Vyombo vya Dola Kutojiingiza Katika Upendeleo wa Kisiasa
- Malawi yazuia Kuingia Kwa Mazao ya Kilimo Kutoka Tanzania Waziri Bashe atoa msimamo wake
- Waziri Ndejembi amrejeshea mjane eneo lake, amwelekeza mkrugenzi kuvunja nyumba iliyojengwa kimakosa
- Zaidi ya Wakazi 12, 000 Wanufaika na Mradi wa Maji wa Mizani- Itete