Wataalam wa Maabara kutoka hospitali mbalimbali nchini, zikiwemo Hospitali za Jeshi, Hospitali za Rufaa Mwanza na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wameaswa kuzingatia kikamilifu mafunzo ya ukaguzi wa maabara zenye ithibati ya ISO ili kuhakikisha uboreshaji endelevu wa viwango vya ubora katika huduma za afya.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dkt. Mbonea Yonazi, alipokuwa akifungua mafunzo hayo ya siku tano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH ambapo ameeleza kuwa washiriki watajifunza mbinu bora za kufanya ukaguzi wa ndani wa maabara, kutoa mapendekezo ya kitaalamu ya kuboresha huduma, na kutekeleza mahitaji ya mifumo ya ithibati kwa ufanisi.
“Mafunzo haya ni fursa muhimu kwa wataalamu wa maabara nchini kujifunza na kuelewa kwa kina viwango vya kimataifa vya ubora. Tunatarajia baada ya mafunzo haya, washiriki wataenda kubadili mwenendo wa utendaji kazi kwenye vituo vyao kwa kuzingatia ubora, usalama na ufanisi,” amesema Dkt. Yonazi.
Aidha, Dkt. Mbonea amebainisha kuwa mafunzo yanayoendeshwa na wataalam kutoka Wizara ya Afya yanatarajiwa kusaidia kuibua wakufunzi wa ndani, ambao baadaye watasaidia MNH kupitia CPL kuwa kituo cha kitaifa cha mafunzo ya ukaguzi wa maabara zenye ithibati na kuifanya MNH kuweza kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wataalam kutoka maeneo mbalimbali nchini hapo baadaye.
Awali, Kitengo cha Huduma za Maabara (CPL) cha MNH kilikuwa na wataalam wawili tu wenye uwezo wa kufanya ukaguzi wa maabara na kupitia mafunzo haya, wataalamu 30 zaidi wataongezwa wakiwemo 20 kutoka MNH-Upanga na 10 kutoka MNH-Mloganzila ambao wataongeza nguvu kazi katika kuhakikisha maabara zinafikia na kuendeleza viwango vya ubora vinavyotakiwa.